Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Tanzania

KOZI YA KIFARANSA

Imewekwa: 09 Jun, 2023
KOZI YA KIFARANSA

Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Tanzania kilichopo Kunduchi Dar es salaam kimeendesha Mafunzo ya lugha ya Kifaransa kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Mafunzo hayo ya awali yameendeshwa kwa muda wiki kumi na mbili kuanzia tarehe 06 Machi 2023 hadi tarehe 07 Juni 23. Mafunzo hayo yamejumuisha Maafisa idadi 23 na Askari idadi 23 ambao jumla yao ni 46. Mafunzo hayo yamefungwa leo na Mkuu wa kituo hicho Brigedia Jenerali George Itang’are. Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Mkuu wa Kituo  hicho alisema, “Ni jambo jema kwa Maafisa na Askari kujifunza lugha zaidi ya moja ili ziwasaidie mnapokuwa kwenye majukumu ya Ulinzi wa Amani’’.

                                               

Mafunzo hayo yanaendeshwa kwa mara ya pili sasa kituoni hapa, ambapo kwa mara ya kwanza yalifanyika mwaka 2022 chini ya Ushirikiano wa Nchi ya Ufaransa Kupitia Ubalozi wake hapa nchini. Madhumuni ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo  Maafisa na Askari katika utekelezaji wa Majukumu yao ya Ulinzi wa Amani hasa katika nchi zinazotumia lugha ya kifaransa. Mafunzo hayo yanatolewa na Mkufunzi kutoka nchini Ufaransa kwa kushirikiana na Wakufunzi wa Kituo. Ushirikiano na Uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Ufaransa unafaida nyingi katika nyanja mbalimbali ikiwemo mafunzo  kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ).