Mafunzo ya Ukufunzi kwa Wakufunzi
Mafunzo ya Ukufunzi kwa Wakufunzi
Imewekwa: 23 Dec, 2022

Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani Tanzania Novemba 28, 2022 kilifunga rasmi Mafunzo ya Ukufunzi kwa baadhi ya Wakufunzi wa Kituo hicho. Washiriki wa Mafunzo hayo ni Maafisa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananch wa Tanzania(JWTZ) wanaofundisha kituoni hapo. Mafunzo hayo yalifungunguliwa Novemba 14, 2022 na yaliendeshwa kwa muda wa wiki mbili.
Aidha mafunzo hayo yaliandaliwa na JWTZ kwa ushirikiano na Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti (United Nations Institute of Training and Research - UNITAR) Akizungumza wakati wa kufunga Mafunxo hayo, Kaimu Mkuu wa Kituo hicho Kanali Deogratias Mulishi aliwashukuru UNITAR kwa kuwezesha Mafunzo hayo kwa Maafisa na Askari wa Jeshi hilo
ReplyForward |